Bingwa mpya wa dunia wa ndondi ya uzani mzito muingereza Tyson Fury amepokonywa taji lake la IBF takriban majuma mawili tangu aitwae.

Kisa na maana shirikisho la kimataifa la masumbwi IBF lilikuwa linataka apiganaje na mpinzani wake anayepigiwa upatu Vyacheslav Glazkov kabla ya kupigana na bondia yeyote yule.

Hata hivyo Fury aliyewatamausha wapenzi wa ndondi za uzani mzito kwa kumchapa bondia kutoka Ukraine Wladimir Klitschko na kutwaa mataji yote matatu ya ndondi ya IBF WBA na WBO.

Pigano hilo la Novemba tarehe 28 lilitamatisha udhibiti wa raia huyo wa Ukraine wa mikanda yote 3 ya ndondi iliokuwa imedumu kwa zaidi ya miaka 10.

Yamkini Fury alilazimika kupigana dhidi ya Wladimir Klitschko kutokana na kipenge cha mkataba waliotia sahihi na bondia huyo wa Ukraine.

Mwenyekiti wa shirikisho la ndondi la kimatafa IBF Lindsey Tucker, aliithibitishia BBC kuwa Fury amepokonywa ukanda huo wa uzani mzito.

”Kwa mujibu wa shirikisho letu Fury alipaswa kuzichapa dhidi ya mpinzani mkuu wa ukanda huu ambaye ni Vyacheslav Glazkov badala yake Fury mwenye umri wa miaka 27 aliamua kutimiza mkataba wa mechi ya marudio dhidi ya Klitschko”

Fury ambaye ameshinda mapigano 25 ya kulipwa amesalia na mikanda miwili ya WBA na ile ya WBO.

Ukanda mwngine wa uzani wa juu WBC unashikiliwa na bondia kutoka Marekani Deontay Wilder.

Kimsingi Ukanda huo wa IBF unarejea Ukraine kwani Glazkov, mwenye umri wa miaka 31 ni raia wa Ukraine,na ameshinda mapigano 21 kati ya 22 alizoshiriki.

Mourinho Na Bosi Wake Wabumba Jambo Chelsea
Azam FC Watekeleza Agizo La Rais John Magufuli