Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kimeingia kambini katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya Morogoro (U-15) mwishoni mwa wiki hii.

U15 inayonolewa na kocha wake Bakari Shime, ianatarajiwa kucheza michezo miwili na timu ya kombaoni ya Morogoro (U15) siku ya jumamosi na jumapili mjini Morogoro, ambapo kocha huyo amekua akitumia nafasi hiyo kupima uwezo wa vijana wake na kuboresha kikosi kwa kuongeza vijana wengine anaowaona wanafaa katika timu hiyo.

TFF imekua na program ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 kukutana kila mwisho wa mwezi kwa kambi, kabla ya kusafiri mikoani kucheza michezo ya kirafiki. Mpaka sasa timu hiyo imeshacheza na timuza kombaini za mikoa ya Mbeya na Zanzibar.

Timu hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, inajandaa na kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Madagascar mwaka 2017.

Rashid Saadallah Kuhojiwa Na kamati Ya Maadili
Taifa Stars Yawasili Salama Uturuki