Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Novemba 22, 2017, katika ofisi za TFF Karume, pamoja na mambo mengine ilijadili shauri la mapingamizi mbalimbali yaliyowekwa na timu za Ligi ya Wanawake.

Timu ya Mburahati Queens iliweka pingamizi kwa mchezaji Ever Kombo ikipinga timu ya Baobab kumtumia kwa kuwa hakulipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.

Kamati imeiruhusu timu ya Baobab kumtumia mchezaji huyo baada ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi hilo.

Aidha Kamati imeiruhusu timu ya Fair Play ya Tanga kumtumia mchezaji Anastazia Mmwacha baada ya timu ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi iliyomuwekea kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.

Kamati imeiruhusu timu ya Panama kumtumia mchezaji Sabina Mbuta aliyewekewa pingamizi na Mburahati Queens kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake,Panama wameruhusiwa kumtumia baada ya kulipa ada hiyo ya shilingi laki moja(100,000).

Timu ya Marsh Academy imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Asfaty Kasindo,Janeth Simba ,Rose Mpoma na Arafa Ramadhan wa Mlandizi Queens,Monica Conrad,Christer J Bahera na Niwael  Makuluta wa Mburahati Queens, Neema Kiniga wa Kigoma Sisters baada ya kukubali kuzilipa timu zao ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake na timu hizo kukubali kuondoa pingamizi.

Nayo, timu ya JKT Queens imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Najiat Abassi,Fumu Ally,Hamisa Athuman wa Ever Green Queens,Fatuma Makusanya na Elizabeth Kadonya wa Mburahati Queens baada ya timu zao kuondoa mapingamizi waliyoweka kwa wachezaji hao kutolipiwa ada ya uhamisho.

Timu ya Simba Queens imezuiwa kuwatumia wachezaji Zainab Rashid wa Ever Green Queens, Grace T Mbelayi, Jackline Kulsanga, Dinna Omary wa Mlandizi Queens, na Halima Hamdani Mchen wa Kigoma Sisters mpaka pale watakapolipa ada ya uhamisho wa shilingi laki moja (100,000) kwa kila mchezaji kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya wanawake.

Mapingamizi yaliyowekwa na timu ya Makongo High School kwa timu mbalimbali ikipinga timu hizo kuwatumia wachezaji wake bila kulipa ada,mapingamizi hayo yametupwa baada ya timu hiyo kushindwa kufika kutetea hoja za mapingamizi hayo.

Timu ya Marsh Academy ya Mwanza imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Zainab Hassan Kienje na Silva Daud waliowekewa pingamizi na timu ya Kigoma Sisters ambayo ilishindwa kufika kwenye kikao cha kujadili pingamizi lake.

Wachezaji Asia Juma,Betista Othuman Abdala na Josephine Julius Nyirenda wameruhusiwa kucheza timu ya Baobab baada ya timu ya Kigoma Sisters iliyowawekea pingamizi kuamua kuyaondoa mapingamizi hayo.

Ndemla afuzu majaribio Sweden
Karia atuma salamu za rambirambi msiba wa Gama