Jeshi la Polisi nchini Nigeria, Jimbo la Kano lilitangaza marufuku ya kutotoka nje kwa saa 24, baada ya Mahakama kubatilisha uchaguzi wa mgombea wa upinzani kama Gavana, na kumtangaza mfuasi wa chama cha Rais Bola Tinubu, kuwa mshindi halali wa Jimbo hilo.

kwa mujibu wa taarifa ya Polisi wa jimbo Kano, ambalo lina wakazi wengi zaidi ya wapiga kura waliojiandikisha, ilisema kWamba watakao kiuka amri ya kutotoka nje watakamatwa na kushughulikiwa kisheria.

Kabla ya uamuzi wa Mahakama hiyo ya uchaguzi, vikosi vya usalama vilichukua udhibiti wa barabara kuu, katika mji mkuu huo wa Kano ambapo uamuzi wa jopo la Majaji watano ulizusha hofu ya kutokea machafuko katika jimbo hilo lenye Waislamu wengi.

Kura ya Ugavana ya mwezi Machi, ilishuhudia Abba Yusuf wa Chama cha New Nigerian Peoples Party akimshinda mgombea wa Chama tawala cha All Progressives Congress, Nasiru Gawuna ambaye alidai kwamba zoezi hilo liligubikwa na udanganyifu.

Simamieni urithishwaji wa ujuzi kwa Wazawa - Rais Samia
Mwalimu mbaroni kwa kumbaka Mwanafunzi