Mchakato uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa, wa kujiandikisha kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa unaanza rasmi leo.

Waziri wa TAMISEMI, Suleimani Jaffo amesema kuwa hatua hiyo itakuwa kipimo muhimu cha kuwapima watendaji kwa jinsi watakavyoufanikisha.

Amesema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa uchaguzi huo , ambao kimsingi ndio sehemu ya awali kuhudumia wananchi katika mgawanyo wa mamlaka ya uongozi wa dola.

Katika hatua hii ya utawala, wananchi huanza kupanga mipango yao ya maendeleo ya jamii kwa ngazi ya mtaa, kijiji au kitongoji.

“Hapa nasisitiza kila mwananchi kwenda kujiandikisha katika eneo lake, kwani hata kama mtu ana kitambulisho cha mpigakura hakitakuwa kigezo cha kumpa uhalali wa kupiga kura katika uchaguzi huo” amesema Waziri Jaffo.

Amesema maandalizi yote muhimu yameshakamilika, vifaa vitakavyotumika katika uandikishaji kama madaftari katika vutuo vyote tayari.

Aidha amesisitiza wananchi kutumia vizuri muda uliowekwa wa siku saba kuhakikisha wanajiandikisha kwenye orodha ya daftari la wapigakura kwani kila atakaye jiandikisha ataweza kugombea nafasi za uongozi na kupiga kura.

Uchaguzi wa Serikali za mitaa unahusisha nafasi mbalimbali, mwenyekiti na wajumbe ambapo kwa mwaka huu utahusisha mitaa 4,294, vijiji 12,319 na vitongoji 64,384.

 

Tim Howard atundika Gloves
Fabian Delph aondolewa kikosini