Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), imetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan la uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa la kwanza ambapo hadi sasa umefikia asilimia 92.
Rais Samia alitoa agizo hilo katika kikao kikichofanyika Ikulu Tarehe 04.01.2021 ambapo alikuwa akipokea taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa maendeleo kwa ustawi dhidi ya UVIKO-19 alionesha kutoridhishwa na kasi ya uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali na darasa na kwanza na kuelekeza viongozi wa TAMISEMI kulisimamia hilo.
Akizungumzia hali ya uandikishaji, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli, amesema zimesalia siku chache kufikia tamati ya uandikishaji wa wanafunzi hao na hali ya uandikishaji kwasasa imefikia asilimia 92.
“Mpaka tarehe 10.02.2022 wanafunzi wa Elimu ya Awali Walioandikishwa ni 1,160,580 (Wav 581,702 Was 578,878)
wakiwemo Wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,347 (Wav 1,188 Was 1,159) sawa na 85% ya kuandikisha wanafunzi wa awali 1,363,834.”
“Na kwa darasa la kwanza Walioandikishwa ni 1,472,517(Wav 734,166 Was 738,351) wakiwemo wenye mahitaji maalum 2,914 (Wav 1,546 na Was 1,368) sawa na asilimia 92.3% ya wanafunzi 1,592,375. wanaotarajiwa kuandikishwa,”amesema
Pia Mweli amebainisha kuwa Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza walioandikishwa ni 751,946 (Wav 370,447 Was 381,499),
Wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 922 (Wav 468 Was 454) sawa na 83% ya wanafunzi waliochaguliwa.
Aidha, amesema kwa upande wa MEMKWA Wanafunzi wa walioandikishwa ni 8,592 (Wav. 4783 na Was 3,809) wakiwemo wanafunzi wenye mahitaji maalum 87 (Wav 41 Was 46).