Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, David Silinde amesema kuanzishwa kwa programu ya vituo atamizi ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuboresha Sekta ya Mifugo kuwa ya kisasa na kuleta tija zaidi.

Silinde ameyasema hayo, wakati wa ziara ya kutembelea vituo atamizi vya Wizara hiyo Mkoani Tanga vinavyotekelezwa kupitia Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa ajili ya kutoa mafunzo ya vitendo ndani ya mwaka mmoja kwa vijana juu ya unenepeshaji ng’ombe katika kipindi cha miezi mitatu.

Amesema, kijana atayakayemaliza pogramu ya unenepeshaji mifugo hususan ng’ombe itakayodumu kwa mwaka mmoja atapatiwa na serikali Shilingi Milioni Kumi za mtaji na kwamba fedha hizo siyo mkopo bali aende kujiendeleza katika ufugaji kibiashara.

Naye Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Angello Mwilawa ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani amesema uwekaji wa miundombinu pamoja na rasilimali chakula cha mifugo kwa gharama za chini nib suala la muhimu.

Wachezaji Simba SC wampa jeuri Robertinho
Mauricio Pochettin anukia Stamford Bridge