Jeshi la Polisi Nchini Kenya limewazuia wananchi waliojitokeza kuingia uwanja wa Kasarani ambapo zinafanyika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule Dkt William Ruto kuwa Rais wa nchi hiyo.

Kutokana na uwanja huo kujaa wananchi wametakiwa kuangalia uapisho huo kupitiatia vyombo vya habari vinavyorusha tukio hilo wakiwa nyumbani.

Ruto aliibuka mshindi katika Uchaguzi mkuu wa Kenya uliofanyika Agosti 9, 2022, na anaapishwa leo kuchukua nafasi ya Rais Uhuru Kenyatta anayemaliza muda wake wa kuingoza Kenya kwa miaka kumi.

Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo Raila Odinga alipinga matokeo hayo katika Mahakama ya Juu nchini humo ambayo ilisikiliza kesi hiyo na kuyatupilia mbali mapingamizi aliyokuwa ameyaweka dhidi ya Ruto.

Hata hivyo Jaji Mkuu Martha Koome alisema Raila na waleta maombi wenzake walishindwa kuthibitisha kulikuwa na udanganyifu na uchakachuaji wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi, siku na baada ya kupiga kura.

Marais waliowahi kuongoza taifa hilo ni Uhuru Kenyatta anayeachia madaraka, pamoja na Daniel Moi na Mwai Kibaki ambao wote wamefariki dunia.

LIVE: William Ruto akiapishwa
Ubunifu na utafiti suluhisho kwa serikali mtandao