Rais wa Urusi, Vladmir Putin ameapa kutoruhusu nchi yake iingie katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuongeza kuwa uasi uliofanywa na kikosi cha mamluki cha Wagner ni uhaini.
Puttin ameyasema hayo, baada ya kiongozi wa kampuni ya mamluki wa kijeshi ya Wagner Yevgeny Prighozin kutangaza kuwa wapiganaji wake, wanadhibiti maeneo muhimu ya kijeshi, yanayoshughulikia mashambulizi dhidi ya Ukraine.
Awali, Mkuu wa kundi la Wagner, Prighozin alisema wapiganaji wake wanadhibiti kituo cha amri za kijeshi na kambi ya anga kwenye mji wa kusini wa Rostov-on-Don, na aliapa kuwapindua viongozi wajuu wa jeshi la Urusi.
Tukio hilo la ghafla, linatoa changamoto kubwa kwa utawala wa Rais Putin na hatari kubwa ya kiusalama tangu alipoingia madarakani mwaka 1999, huku Prigozhin akisema Rais Putin anafanya kosa kubwa kumtuhumu yeye na kundi lake kwa usaliti.