Matukio ya ubakaji wa watoto wilaya ya kibiti mkoani pwani yamekuwa tishio kwa kuongezeka mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, Gulam Hussein ambaye ametaja wilaya hiyo kuwa inakabiliwa na kesi nyingi za watoto kupata ujauzito kwa kubakwa.
Gulam ameyasema hayo mbele ya madiwani, katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wilayani Kibiti, pia ameongeza kuwa licha ya Kibiti kukabiliwa na kesi nyingi za kubakwa kwa watoto na kupewa minba lakini viongozi wa vijiji hukaa vikao na familia na kumalizana bila kuwafikisha wahusika mahakamani.
“viongozi wa vijiji ambao wanashirikiana na watu waliotenda makosa ya ubakaji na kuwapa mimba watoto na kushindwa kuwafikisha mahakamani sheria zichukuliwe dhidi yao” aliongeza.
Na kuwataka wazazi ambao wanawaozesha watoto wao nao wachukuliwe hatua.
Licha ya mkuu huyo wa wilaya ya Kibiti kusisitiza na kutoa agizo, hatua kuchukuliwa kwa wabakaji na amewasihi wananchi kukumbuka kuwa haki ya mtoto ni kupata elimu na sio kufanyiwa vitendo vya ukatili.