Ubalozi wa China Tanzania umetoa msaada wa vifaa kinga ili kukabiliana na mlipuko wa Corona Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia waathirika, barakoa (mask) 100,000 na vipima joto vya mkono 150
Balozi Wang Ke amesema China imejikita kuisaidia Tanzania katika misaada ya dharura katika kukabiliana na Virusi vya Corona, Ameongeza kuwa Tanzania na China wamekuwa marafiki kwa muda mrefu na Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kusaidia China ilipokumbwa na janga hilo.
Akipokea msaada huo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa shukrani kwa Ubalozi wa China na kusema vifaa kinga hivyo vitawasaidia watumishi wa afya nchi nzima, ili kuwakinga wasipate maambukizi ya Corona pindi wanapo hudumia waathirika
Hata hivyo Kampuni ya Twiga iliyoundwa kwa Ubia wa Serikali na Barrick Gold Corporation nayo imetangaza kutoa msaada wenye thamani ya Dola Milioni 1.7 (takriban Bilioni 4) ambao utakuwa katika mfumo wa vifaa na utaalamu ili kusaidia kudhibiti maambukizi ya Corona.