Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani kupitia kwa balozi wake, Abdallah Possi umejibu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Singida Mashariki, kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu alipofanya mahojiano na kipindi cha DW News Africa kilichorushwa mnamo Januari 28, 2019.
Ubalozi huo umeomba nafasi katika kituo hicho ili uweze kujibu mashambulizi ya Lissu lakini kabla hawajapangiwa muda wa kwenda kuzungumza wameona waweke mambo kadhaa sawa.
Ubalozi huo umesema kuwa unasikitishwa sana na kitendo cha Lissu ambaye yuko kwenye matibabu, kuzunguka katika nchi za kigeni akitoa tuhuma nzito dhidi ya nchi yake, huku Watanzania hususani wananchi wa Jimbo lake ambao wanategemea arudi nchini ili aendelee kuwatumikia.
Aidha, katika taarifa hiyo, ubalozi umesema kuwa si sahihi kwa Lissu kuubadiri wema kuwa ubaya kwasababu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alitoa tamko la kulaani shambulizi na pia kuagiza upelelezi wa kina ufanyike, huku akimtuma Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Rais mstaafu Alli Hassan Mwinyi na viongozi wengine wakubwa kwenda kumtembelea Lissu hospitalini Dodoma, Nairobi na Brussels.
Hata hivyo, taarifa hiyo ya Ubalozi imeongeza kuwa vyombo vya dola vimefanya na vinaendelea na upelelezi lakini ni lazima Lissu na dereva wake kama mashahidi wakuu watoe ushirikiano ili kuukamilisha upelelezi huo ambapo mpaka hadi sasa Mbunge huyo hajatoa ushirikiano kwa Polisi
Pia kuhusu kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe taarifa hiyo imesema hajafungwa bali dhamana yake ilisitishwa na Mahakama kutokana na yeye kukiuka masharti
-
Wangabo atoa wiki tatu kwa Wajasiliamali Sumbawanga
-
Benki ya Dunia yatoa Bilioni 21.7 kuboresha miundombinu Mtwara
-
Umuhimu wa barua bora ya maombi ya kazi katikati ya maelfu ya waombaji