Taifa la Ubelgiji limefanikiwa kufika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora wa soka duniani kwa mwezi Oktoba, na kuishusha Ufaransa ambayo bado inaendelea kukumbukwa, kufuatia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa dunia mwezi Julai mwaka huu.

Ubelgiji imekwea kileleni kwa kuizidi Ufaransa alama moja, kufuatia kufanya vyema katika michezo ya kimataifa waliyocheza mwezi huu (Michuano ya ligi ya mataifa barani Ulaya “UEFA Nations League”), pamoja na michezo ya kirafiki.

Katika michezo hiyo Ubelgiji iliifunga Uswiz katika michuano ya UEFA Nations League na baadae kulazimishwa sare na Uholanzi kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

Kwa upande wa Ufaransa waliifunga Ujerumani katika michuano ya UEFA  Nations League, na kabla ya hapo walilazimishwa sare na Iceland katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.

A graphic demonstrating the new FIFA/Coca-Cola World Ranking

Taifa la Brazil, limeendelea kuwa taifa pekee mbali na mataifa mengine ya Ulaya yanayoendelea kutawala kwenye kumi bora za orodha ya viwango vya ubora wa soka duniani.

Hata hivyo katika orodha iliyotolewa hii leo na shirikisho la soka duniani FIFA, taifa lililopanda kwa kiwango kikubwa ni Gibraltar, kufuatia timu yake kupata ushindi katika michezo yake miwili kwa mwezi Oktoba.

Taifa la Gibraltar, ambalo lilijiunga na FIFA mwaka 2016, limepandwa kwa nafasi nane na kukamata nafasi ya 190, kutokana na ushindi dhidi ya Armenia na Liechtenstein katika michuano ya UEFA Nations League.

Madagascar, ambao wamefuzu fainali za Afrika 2019 mapema mwezi huu, nao wamepanda na kuingia kwenye orodha ya 100 bora tangu mwaka 2002. Taifa hilo la kusini mwa Afrika limepanda kwa alama 6 kutoka 106 hadi 100.

Taifa la Tunisia linaendelea kuwa kinara katika ukanda wa bara la Afrika, kwa kushika nafasi ya 22 kwa ubora duniani, huku Iran inayoshika nafasi ya 30 katika viwango hivyo, ikiwa kinara upande wa bara la Asia.

Tanzania ambayo ilipoteza mchezo dhidi ya Cape Verde kwa kufungwa mabao matatu kwa sifiri mjini Praia kabla ya kuvibanjua visiwa hivyo mabao mawili kwa moja siku nne baadae jijini Dar es salaam mwezi huu, imepanda kwa nafasi nne kutoka 140 hadi 136.

Kuangalia orodha kamili ya viwango vya ubora wa soka duniani bofya hapa

 

Makampuni 10 yatangaza nafasi za kazi, 'Apply' hapa
Al Masry wasusa DR Congo, waipeleka AS Vita Club fainali