Mwenyekiti wa CCM mkoani Morogoro, Innocent Kalogeresi ameahidi kuyarudisha majimbo matatu ya ubunge yaliyochukuliwa na upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ametoa ahadi hiyo mara baada ya kuchaguliwa kuongoza kwa mara nyingine tena mkoa huo, ambapo amesema kuwa majimbo hayo yalichukuliwa kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wa CCM na kutokuwa na umoja.

Aidha, ameyataja majimbo yaliyochukuliwa na Chadema, ni pamoja na Mikumi, Kilombero na Mlimba ambayo yalichukuliwa na chama hicho.

“Na hata Kata zilizochukuliwa na upinzani nawahakikishia zinarudi zote, naomba viongozi wenzangu tushirikiane tuache ubinafsi, tutangulize maslahi ya chama mbele,”amesema Kalogeresi

Hata hivyo, amewata wana- CCM wote kuweka maslahi mbele ya chama kuepuka ubinafsi na migogoro isiyokuwa na tija.

Facebook yawafungulia milango watoto kujiunga
Video: Makachero Polisi uso kwa uso na Lissu Nairobi, Askofu Gwajima abomoa kanisa lake