Timu za soka za Yanga na Azam FC usiku wa leo (Jumanne) zitashuka kwenye uwanja wa Amaan kumenyana katika mchezo wao wa pili wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Yanga inaikabili Azam huku ikiwa tayari ina pointi tatu na mabao matatu ya kufunga baada ya ushindi wa 3-0 iliyoupata juzi dhidi ya Mafunzo.

Azam FC itashuka dimbani huku ikiwa na pointi moja iliyopata juzi baada ya sare ya 1-1 na Mtibwa Sugar.

Mechi hiyo huenda ikavuta hisia za wengi huko Zanzibar kufuatia timu hizo kubadilishana nafasi ya kwanza na ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu bara.

Mchezo huo ambao utaanza saa 2:15 usiku utatanguliwa na mchezo kati ya Mtibwa na Mafunzo ambao utaanza saa 10:15 jioni.

Magufuli afuta hati ya Ardhi ya Mwekezaji na kuwakabidhi wananchi
Mbabe Wa Francis Cheka Asakwa Na Polisi Jijini Dar es salaam