Kutokana na uchakavu wa kiwanda cha kuzalisha Kahawa cha TANICA, ambacho kinamilikiwa na Vyama vya Ushirika na Serikali nchini, jitihada za kusaidia uboreshaji wa miundombinu bora ya uzalishaji wa zao hilo umeanza.

Akizungumza katika ziara ya kufuatilia na kuangalia mikakati ya uongozi wa kiwanda hicho, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amekiri uchakavu wa miundombinu ya kiwanda hicho na kusema Serikali itawekeza fedha kwa ajoli ya kutengeneza mazingira bora ya uzalishaji.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila (wa pili kutoka kulia), na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto sima (wa tatu kutoka kulia), wakikagua bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha TANICA.

Amesema, “ni kweli kwamba kiwanda chetu kwa sasa kina mitambo chakavu, na hili lazima sasa tulibebe vizuri ili kuhakikisha kwamba angalau serikali inaweka pesa kama ambavyo pia wamehaidiwa kilichobaki ni sisi kuendelea kufanya kazi vizuri ili mwisho wa Siku kiwanda chetu kisife.”

Licha ya kiwanda hicho kuwa kwenye ukarabati mpaka sasa, zaidi ya bilioni 51 zinahitajika kuboresha miundombinu ya kiwanda hicho kama Katibu tawala msaidizi sehemu za uchumi na uzalishaji ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Isaya Tendega alivyobainisha.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila na viongozi wa kiwanda cha TANICA, wakikagua moja ya mashine za kuchakata Kahawa.

“Uhitaji ni mkubwa katika upanuzi wa kiwanda hiki na mikakati waliyonayo uongozi wa kiwanda ni kuwekeza zaidi ya bilioni 51 kwaajili ya upanuzi, ujenzi na ununuzi wa mitambo mipya kwasababu iliyopo ni yamda mrefu na imechakaa,” amebainisha Tendege.

Naye Meneja Mkuu wa kiwanda cha TANICA, Mhandisi Rodness Milton amesema, ” kwa sasa hivi kutokana na uchakavu uliopo tunaweza kuzalisha 60% ambayo ni takribani tani 300 kwa mwaka, kwahiyo kuna 40% inapotea kutokana na uchakavu huo.”

Juma Mgunda: Tunaifuata Azam FC Mtwara
Mayele aunguruma Singida, alama tatu lazima