Waziri wa mawasiliano na uchukuzi, Rahma Kassim amesikitishwa na ubovu  wa mashine ya meli ya MV Mapinduzi II.

Amesema hayo wakati alipofanya ziara katika taasisi zilizo chini ya wizara yake ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.

Amesema anasikitishwa na meli ya MV Mapinzuzi II kushindwa kuendelea kwa shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo kwa muda wa miezi miwili sasa na kila siku meli hiyo inagharimu million nne kwa siku kwa ajili ya mafuta.

Nae injinia wa meli hiyo Mwinyi Ramadhan amemueleza Waziri kuwa jambo linalopelekea meli hiyo kuharibika mara kwa mara ni kuwa meli hiyo ilinunuliwa na kukabidhiwa ikiwa na mashine mbovu.

Aidha ameutaka uongozi wa shirika la meli kuwasili wizarani  kwa lengo la kukaa pamoja na kuweza kulijadili tatizo hilo ili meli hiyo iweze kufanya safari zake za Unguja na Pemba.

Kocha Kaze aahidi soka safi Azam Complex
Cioaba: Tupo tayari kuikabili Young Africans