Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imemuonya mgombea urais wa Tanzania kupitia chama vha ukombozi wa umma (CHAUMA), Hashimu Rungwe kuhusu ahadi yake ya kuwapa ubwawa wananchi watakaohudhuria katika mikutano yake ya kampeni za uchaguzi mkuu.

Mkuu wa TAKUKURU wilaya ya Ilala , Christopher Myava , ametoa onyo hilo jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam akisema kugawa chakula hicho ni kosa kisheria na ni rushwa.

Wakati TAKUKURU ikitoa onyo hilo, mgombea huyo amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wake na kwamba ubwabwa utakuwepo.

Myava amesema katika kipindi hiki anachotakiwa kufanya mgombea ni kuomba ridhaa ya wananchi kumchagua na si kushwawishi kwa kutoa rushwa.

Rungwe anatarajiwa kuzindua kampeni zake leo Manzese, wilaya ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Majaliwa: Chama chetu hakikurupuki
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 5, 2020