Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), imewataka wagombea ubunge na udiwani waliokata rufaa kuwa na subra wakati rufaa hizo zikishughulikiwa.

Hayo yamesemwa leo Septemba 15, na mkurugenzi wa uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera Charles, wakati akifungua mkutano wa tume hiyo na watoa huduma ya habari mtandaoni unaofanyika jijini Dar es Salaam.

”Wanapokuwa wanatoa matamko yao kuwa tunachelewa kutoa uamuzi wa rufaa, watambue tunazifanyia kazi kwa kuzichambua kwa kina ili tuweze kutenda haki,” amesema Dkt Mahera.

Kauli hiyo ya Dkt. Mahera inakuja siku moja baada ya katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), John Mnyika kuitaka tume hiyo kutoa majibu ya rufaa hizo haraka ili wagombea waanze kampeni.

Aidha, NEC imetoa onyo kwa wanasiasa wanaotoa lugha zisizostahili kwenye majukwaa ya kampeni kuwa tume itawachukulia hatua ikiwemo kusitisha mikutano yao ya kampeni.

Dkt. Mahera pia ametangaza kuwa NEC imekubali rufaa 24 za wagombea udiwani kati ya rufaa 49 na kuwarudisha wagombea katika kinyanganyiro hicho.

Michael Sarpong aivulia kofia VPL
Membe kuanza kampeni rasmi Tabora

Comments

comments