Nyota wa zamani wa soka George Weah na makamu wa rais Joseph Boake, wanaelekea duru ya pili ya uchaguzi kwenye uchaguzi wa rais nchini Liberia.

Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini Liberia kura zote zimehesabiwa na George Weah anaongoza kwa asilimia 39 huku Boakai akiwa wa pili kwa asilimia 29.

Mshindi katika kinyang’anyiro hicho analazimika kujipatia asilimia 50 ya kura zote ili aweze kutangazwa mshindi wa uraisi hivyo kutokana na wagombea wote kushindwa kufikisha asilimia 50 ya kula zilizopigwa inalazimika kuwepo kwa uchaguzi wa marudio.

George Weah ambaye ni muafrika wa kwanza kushinda tuzo ya mpira wa miguu yaa Ballon D’Or na Joseph Boakai wote walikuwa wametabiriwa kuwa wangeshinda duru ya kwanza lakini matokeo yamekuwa tofauti kwani wote wameshindwa kupata ushindi wa asiliamia 50.

 

JPM amtumbua Hassan Kibelloh, afanya uteuzi upya
Video: Sababu za usalama zamkwamisha Lowassa, Wahamiaji haramu sasa pasua kichwa