Mgombea wa Republican ambaye pia ni Gavana wa Jimbo la Texas, Ted Cruz amemshinda mpinzani wake Donald Trump katika kura za mchujo  wa chama hicho katika jimbo la Lowa, ikiwa ni mbio za kuelekea katika uchaguzi Mkuu wa Marekani utakaofanyika Novemba mwaka huu.

Matokeo hayo yameamsha ari mpya kwani Trump ndiye aliyekuwa anapewa nafasi nafasi ya juu zaidi kwa chama chake na sasa amewekwa katika nafasi ya pili.

Trump amempongeza Cruz kwa ushindi huo na kueleza kuwa ameridhika kabisa na matokeo yanayomfanya kushika nafasi ya pili.

Kwa upande wa Democratic, asilimia 95 ya matokeo yaliyotangazwa yanaonesha kuwa Hillary Clinton na mshindani wake Bernie Sanders wanatofautiana kwa asilimia 1% ya kura zote.

Bi. Clinton aliwahutubia watu wanaomuunga mkono lakini hatutangaza ushindi wake. Badala yake aliwaeleza kuwa ameshusha pumzi inayompa unafuu.

 

Zitto awasha moto ufisadi wa Trilioni 6.8
WHO yatangaza hali ya hatari duniani kwa ugonjwa wa Zika sawa na Ebola