DAKIKA 90 – KARIAKOO DERBY
Dakika 45 za kipindi cha kwanza bora kwa Yanga SC, Yani ile mpira umeanza Yanga walikuwa kweli kweli wameianza mechi, walicheza kiume, hawakutaka kuwa slow, walienda kwa nguvu
Simba hawakuweza kutuliza presha ya Yanga mpaka wanafungwa goli, hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa la Simba na ubora maridadi wa Yanga
Feisal Salum alicheza kwa kuheshimu nafasi yake, alivizia pocket space sana, kila Yanga walipopora mpira aliuomba kwa haraka na kugeuka
Kwa jinsi Yacouba alivyokuwa akikimbia, amewapa sana mabeki wa Simba, dakika mbili kulia mara kushoto mara kati, hii ni nightmare kwa Beki yeyote
Kiufupi Yanga kipindi cha kwanza walikuwa na wakati mzuri, walipiga progressive passes ila Simba walipiga possessive passes, faida hapo ni kwa wananchi
Kipindi cha pili kumbe Simba walichokuwa wanakitafuta walikuwa wamekikalia, akaingia Bwallya, huyu ndie aliipa Simba walichofikiria sio walichocheza
Mechi ikaamia kwa Simba, kwa upande wao walifanya kila kitu ila hawakufunga goli
Kama ilivyo kawaida ya mapacha hivi karibuni, kipindi cha kwanza alikichukua Yanga na cha pili alichukua Simba, ila Yanga wao hawakukichezea walikitumia, Simba alikichukua na kukipapasa
Kwa mara nyingine tena tunakuja kuona wananchi wanawazidi Simba kwenye swala la kujitoa, achilia mbali mbinu, hizo tupa kule
Ila pale Simba alipotaka goli Yanga alimpiga pini na kuzuia kwa nguvu, ila pale Yanga alipotaka goli Simba alishindwa kuhimili na Yanga alilipata
NB: Hata mkichukua ubingwa ila ubingwa ni butu ?
Imeandikwa na @danirito_thomson