Nchini Kenya mjadala unaendelea kufuatia kiongozi wa upinzani Raila Odinga kujiondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu.

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu je uchaguzi utafanyika au mgombea aliyebaki Rais Uhuru Kenyatta atangazwe kuwa mshindi bila kufanyika uchaguzi.

Tayari Rais Uhuru Kenyatta amesema pamoja na kujiondoa Raila Odinga wa NASA uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa.

Uchaguzi nchini Kenya unatarajiwa kufanyika tarehe 26 na utakuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama kuu nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

 

Diamond afanya video ya ngoma mpya na Rick Ross
Country Boy kuja na albam yenye 'watu wazito'