Nguzo ya uchumi jumuishi wa kidigitali, inakusudia kupunguza na hatimae kuondoa pengo baina ya watu wanaofikia na kutumia huduma za Kidigitali na wasiopata fursa hiyo inayoweka msingi wa kushughulikia vikwazo vya kupata elimu na mafunzo ya TEHAMA kwa jamii, ikilenga kuhakikisha kila mtu ananufaidika na uchumi wa kidigitali.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Kakele wakati akifungua Mkutano wa wanawake kwenye Kongamano la Saba la Tehama Tanzania, lililoandaliwa na Tume ya Tehama, chini ya uongozi wa Dkt. Nkundwe Mwasaga.

Amesema, “mtakubaliana nami kwamba ili maendeleo yaweze kuwa na maana hayana budi kufangamanishwa moja kwa moja na watu. Aidha, kigezo muhimu cha watu, ni kufikiwa kwa makundi yote katika jamii pasipo ubaguzi wa aina yoyote. Katika muktadha huu, ili kujenga msingi wa maendeleo endelevu, matumizi ya TEHAMA kama nyenzo wezeshi hayana budi kufikia makundi yote katika jamii.”

Kakele pia aliwataka Wanawake kutumia jukwaa hilo kupaza sauti kama Taifa ili kuweza kujadiliana kuhusu vikwazo vinavyowakabili juu ya uchangamkiaji wa matumizi ya Teknolojia na TEHAMA, katika shughuli zao za kila sikukwani wao na Vijana wana nafasi maalumu ya kuongoza harakati za kupinga matumizi mabaya ya TEHAMA.

“Sisi kama Wizara yenye dhamana ya TEHEMA hapa nchini, tungependa kusikia sauti zenu, mkielezea fursa zilizopo na changamoto za matumizi ya TEHEMA. Aidha, tutafurahi kusikia kuhusu mawazo yenu, maoni yenu na matarajio yenu kwa serikali juu ya nini kifanyike ili kuendelea kujenga mazingira mazuri na rafiki kwa wanawake kufikia na kutumia teknolojia zinazoibukia,” aliongeza.

Nguzo ya uchumi jumuishi wa kidigitali, inakusudia kupunguza na hatimae kuondoa kabisa pengo baina ya watu wanaofikia na kutumia huduma za kidigitali na wasiopata fursa hiyo (digital divide). Aidha, nguzo hii inaweka msingi wa kushughulikia vikwazo vya kupata fursa ya kupata elimu na mafunzo ya TEHAMA kwa jamii. Lengo ni kuhakikisha kwamba kila mtu pasipokujali hali yake au sehemu anayotoka anashiriki na kufaidika na uchumi wa kidigitali.

Utatuzi changamoto za Muungano unaendelea - Dkt. Jafo
Rais Samia azungumza na Kardinali Rugambwa