Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima , ameitikia wito na kufika katika Ofisi za Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania – UWT, Makao Makuu Jijini Dodoma, ambapo amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Jokate Mwegelo.

Gwajima ameitikia wito wa Jumuiya hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Taifa Mama Mary Chatanda (MCC) , wa kumtaka kufika ili kuzungumza na kujadili juu ya agenda mbalimbali zinazowahusu Wanawake.

Agenda hizo ni pamoja na masuala ya Kiuchumi, Kisiasa, Ukatili wa Kijinsia na Mipango mbalimbali iliyopo katika kuimarisha Jumuiya na kuendelea kumkomboa Mwanamke Kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwa ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha, pia wamejadili kuendelea kuhakikisha Wanawake wanainuliwa kiuchumi ikiwa ni dhamira thabiti ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan , katika kujenga na kuimarisha Jamii iliyo bora na rafiki kwa Watoto na Wanawake wote Nchini.

TMA yatoa tahadhari ya mvua kwa siku nne
Serikali yawatoa hofu Wananchi, taarifa mgonjwa mpya wa Surua