Licha ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja na Umoja wa Mataifa, Korea Kaskazini imezidi kuimarika kiuchumi kwa haraka zaidi katika kipindi cha miaka 17 iliyopita licha ya kuwekewa vikwazo kutokana na mpango wake wa kinyuklia na utengenezaji wa makombora ya masafa marefu.
Ukuaji wa uchumi huo unatokana na ongezeko la Uzalishaji wa bidhaa nchini humo kwa asilimia 3.9 mwaka 2016 ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo ukuaji huo unatokana na uchimbaji madini kawi na uuzaji wa bidhaa nchini China.
Aidha, Marekani imekuwa ikiitaka Beijing kukata biashara na Pyongyang huku wasiwasi ukiongezeka kuhusu mipango ya kinyuklia ya rais, Kim Jong Un, baada ya kuzidisha majaribio mbalimbali ya makombora ya masafa marefu.
Hata hivyo, China ndio mshirika mkuu wa Korea Kaskazini na mfadhili mkuu wa misaada nchini humo huku hatua hiyo ikipingwa vikali na Marekani ambayo inashawishi kutengwa kwa Korea Kaskazini.