Mamlaka Huru ya Kusimamia Polisi nchini Kenya (IPOA), imeanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya mwanahabari mashuhuri wa Pakistani, Arshad Sharif.

Mkuu wa IPOA, Ann Makori, amewaambia waandishi wa habari jijini Nairobi kuwa timu maalum ya kutafuta majibu ya haraka imeanza kuchunguza mauaji hayo ili kubaini ukweli.

Arshad Sharif aliuawa na Polisi kwa kupigwa risasi ya kisogo iliyotokeza katika paji la uso usiku wa Jumapili (Oktoba 23, 2022), katika kaunti ya Kajiado, iliyopo jirani na mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Bruno Shioso alisema mwanahabari huyo aliuawa katika kizuizi cha barabarani kuu ya Nairobi-Magadi kwaa utambulisho wa kimakosa.

Rais wa Pakistan, Arif Alvi amesema kifo cha Arshad Sharif ni pigo kubwa kwa tasnia ya uandishi wa habari nnchini kwake, huku akimuombea apumzike kwa amani.

Safari ya Simba Queens kwenda Morocco yaiva
Kocha Simba SC atamba kuitibulia Young Africans