Waombolezaji waliofika katika mazishi ya ajuza mmoja nchini Ecuador, wamepigwa na butwaa baada ya kugundua kuwa marehemu bado alikuwa hai, licha ya awali madaktari kuthibitisha na kutangaza kuwa alifariki.

Ajuza huyo, Bella Montoya (76), alitangazwa kufariki wiki iliyopita baada ya kuugua Kiharusi kilichopelekea umauti wake ambapo baadaye majira ya saa tano, usiku wa kuamkia Ijumaa (Juni 9, 2023), familia ikijiandaa kubadilisha nguo zake kabla ya mazishi, ilipatwa na mshangao walipomkuta akipumua.

Kwa sasa Bi Montoya amerejeshwa hospitalini kwa uangalizi zaidi, huku Wizara ya Afya ya Ecuador ikiunda kamati kuchunguza tukio hilo la ajabu lililotoea nchi hiyo iliyopo Magharibi mwa Pwani ya Amerika Kusini.

Kupitia taarifa, wizara hiyo ilisema kwamba mwanamke huyo alipatwa na mshtuko wa moyo na baadaye kushindwa kupumua na walipojaribu kumuamsha haikuwezekana na daktari wa zamu akathibitisha kifo chake mbele ya Mwanawe, Gilber Rodolfo Balberán Montoya.

Shirikianeni kukamilisha miradi ya maji kwa wakati - Majaliwa
Majambazi wanne wauawa na Polisi, mmoja atoroka