Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kuwa lina mashaka kuhusu uhalali wa udaktari wa mtu mmoja anayedaiwa kuwa tajiri aliyeshinda katika mnada wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi uliofanyika siku ya Alhamisi kwa kuwa ameshindwa kuonyesha vielelezo vya kuthibitisha elimu yake ya kiwango cha Ph.D.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa     wanaendelea na upelelezi dhidi ya mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Dkt. Louis Shika na kwamba jana hiyo walikwenda kumkagua nyumbani kwake Tabata Mawenzi.

Amesema kuwa Shika hana taaluma ya udakatri na kwamba inasemekana huenda alitumwa na Mfanyabiashara Lugumi mwenyewe kuharibu mnada huo baada ya kushindwa kutoa fedha ambazo alidai ziko nje ya nchi.

“Tulipokea taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Stanley Kevela, kuwa huko Mbweni JKT wakiwa wanafanya mnada wa hadhara wa kuuza nyumba za mfanyabiashara Lugumi, alijitokeza mtu anayeitwa Shika ambaye alishinda mnada huo kwa kutaka kununua nyumba zote tatu, kumbe hakuwa na fedha,”amesema Mambosasa

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema kuwa taarifa zinaonyesha kuwa inawezekana mtu huyo alitumiwa na Mfanyabiashara Lugumi mwenyewe kwa kuwa alivyotakiwa kutoa fedha alisema ziko nchini Russia na Lugumi hajulikani mahali anapoishi kwa sasa.

 

Diamond afunguka ujio wa ngoma yake na Rick Ross
Sadio Mane aipeleka Senegal kombe la dunia