Leo April 13, 2018 Shirika la Mawasiliano Tanzania la (TTCL), limetangazwa kuwa ndio litakuwa linatoa huduma ya tiketi na kusimamia mfumo wa kielektroniki wa mabasi ya mwendokasi baada ya mkataba wa Maxcom Afrika na UDART kumalizika.
Akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu mabadiliko hayo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano, UDART, Deus Bugaywa amesema mkataba baina ya UDART na Maxcom umeisha.
Bugaywa amesema mkataba huo umemalizika baada ya kudumu nao kwa muda wa miaka 2, ambapo wameamua kusaini mkataba mwingine na TTCL.
“Sababu kubwa ni kwamba tumemaliza mkataba nao, hii ni kawaida kama ilivyo kwa kampuni zinavyofanya, ambapo tumempata ubia mpya ambaye ni TTCL,” -Bugaywa.
Pia Bugaywa amesema kuwa mabadiliko hayo yanaweza kusababisha usumbufu katika siku chache kuanzia sasa kutokana mfumo huo mpya wa TTCL.
“Nawaomba watumiaji wa usafiri huu wawe na imani kwani tunaamini mabadiliko haya yatakuwa ya kisasa,”