Klabu ya daraja la kwanza, Geita Sport Club imepata udhamini wa milioni 300 kutoka kwa Kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mine. Klabu hiyo ambayo imepanda daraja la kwanza msimu huu imepania kucheza ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/17.
Klabu hiyo ya Mkoa Mpya wa Geita iko kambini kwa Miezi miwili sasa kuelekea msimu mpya wa FDL. Timu hiyo imekuwa ‘ ikiungwa mkono’ na wanakazi wa Geita, viongozi wa chama cha soka na serikali ya mkoa imesaini mkataba mwaka mmoja na kampuni hiyo ya uchimbaji wa madini. Ni udhamini ghali zaidi katika ligi daraja la kwanza Tanzania Bara.
Ni kitu kikubwa si tu kwa Mkoa wa Geita bali ni ishara njema kwa mpira wa Tanzania kwa kuwa sasa tunaizungumzia timu mpya ya daraja la kwanza ikiwa na udhamini ambao hata baadhi ya klabu za ligi kuu hazijawahi kupata.
Nitashangaa kama klabu nyingine zitaisema vibaya timu hiyo pindi ikianza kufanya vizuri kwa kuwa tayari wako kambini kwa zaidi ya Miezi miwili na sasa wamepata kitu kikubwa zaidi ambacho ni udhamini utakaorahisisha upatikanaji wa mahitaji yote muhimu katika timu.
Shukrani kubwa kwa chama cha soka na serikali ya wilaya ambao wamekuwa wakiisapoti timu hiyo tangu ikiwa katika ligi za chini. Ni ushawishi mkubwa ulitumika ili kuifanya kampuni hiyo ya uchimbaji kuafiki kuidhamini Geita Gold Sport.
Sasa ni kuzifanya pesa hizo kuwahudumia wachezaji kwa kuwalipa vizuri ili wacheze mpira, kuendesha kambi ya timu na mambo mengine mengi.

Ukawa, CCM Wagombea TV Kurusha Matangazo ‘Live’ Jumamosi Hii
TFF Yatuma Salamu Za Pongezi Kwa Bayi