Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM, kimethibitisha kifo cha Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya Sanaa katika Elimu, katika Ndaki ya Insia na Sayansi ya Jamii, Nusura Hassan Abdallah ambaye tangu mwanzoni mwa wiki taarifa zake zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya jamii.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha masoko na mawasiliano Mei 5, 2023 imesema Mei 3, 2023 menejimenti ya chuo hicho ilipokea taarifa kutoka kwa mwanafunzi anayesoma naye kuwa amepokea taarifa kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa mjomba wake Nusura akimjulisha kuwa mwanafunzi huyo amefariki dunia.

Mtu huyo alisema Nusura alifariki wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Faraja iliyopo Himo mkoani Kilimanjaro ingawa hadi kufikia Aprili 27, 2023 Nusura alionekana chuoni akiendelea na masomo.

Taarifa hiyo imesema, mwili wa marehemu ulisafirishwa Mei 3, 2023 kutoka Moshi hadi nyumbani kwao Iramba mkoani Singida na kwamba Menejimenti ya chuo hicho imesikitishwa na msiba huo na inatoa pole nyingi kwa familia ya marehemu Nusura.

Tunachunguza kifo cha Nusura - Misime
Habari Picha: Sherehe kusikimwa ufalme, Charles wa III