Wawakilishi pekee wa England kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya nusu fainali, klabu ya Man City wamepangiwa kukutana na mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo Real Madrid.

Man City wamepangwa na Real Madrid kupitria droo iliyofanyika muda mchache uliopita kwenye ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka barani Ulaya huko mjini Nyon nchini Uswiz.

Mchezo mwingine wa hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu, utashuhudia mabingwa wa soka kutoka nchini Ujerumani FC Bayern Munich wakipapatuana na Atl├ętico Madrid kutoka nchini Hispania.

Michezo ya mkondo wa kwanza ya hatua hiyo itachezwa April 26/27 na kisha michezo ya mkondo wa pili itaunguruma Mei 3/4.

Simba Kushiriki Michuano Ya Nile Basin
Siri Ya Athumani Iddi Chuji, Jerry Tegete Kukaa Benchi Yafuchuka