Shirikisho la Soka Barani Ulaya ‘UEFA’ linaendelea kupinga kuanzishwa kwa michuano ya European Super League, ambayo itakuwa ikifanyika kati kati ya juma.

Fukuto la kuanzishwa kwa michuano hiyo limepamba moto tangu jana Jumatatu, ambapo klabu 12 za barani humo zimekutana na kuafiki kujitenga na kuanzisha European Super League, ambayo itakuwa mpinzani mkubwa wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ‘UEFA Champions League’.

Klabu 12 zilizokubali kuanzisha michuano ya European Super League ni AC Milan, Arsenal FC, Atlético de Madrid, Chelsea FC, FC Barcelona, FC Internazionale Milano, Juventus FC, Liverpool FC, Manchester City, Manchester United, Real Madrid CF na Tottenham huku vilabu vitatu vikitarajiwa kuongezeka lakini PSG, Bayern Munich na Borrusia Dortmund zikikataa kujiunga katika Ligi hiyo.

UEFA wametoa taarifa ambayo inaendelea kuonesha kupinga kuanzishwa kwa michuano hiyo ambayo inaeleza kuwa: “Tutachukua hatua zote zinazowezekana kwetu, katika viwango vyote, kimahakama na michezo ili kuzuia kutokea. Kandanda inategemea mashindano ya wazi na sifa ya mchezo; haiwezi kuwa kwa njia nyingine yoyote.

“Klabu zinazohusika zitapigwa marufuku kucheza kwenye mashindano mengine yoyote katika ngazi ya ndani, Ulaya au ulimwengu, na wachezaji wao wanaweza kunyimwa nafasi ya kuwakilisha timu zao za kitaifa.”

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 21, 2021
Morrison kuikosa Kagera Sugar