Kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, imebariki adhabu iliyotangazwa na shirikisho la soka duniani FIFA kupitia kamati ya maadili dhidi ya rais Michel Platini.

Kamati ya utendaji ya UEFA, imebariki maamuzi yaliyochukuliwa dhidi ya kiongozi huyo kwa kuheshimu adhabu ya kufungiwa kwa siku 90 iliyotangazwa na FIFA hapo jana, ili kupisha uchunguzi ambao utafanywa na serikali ya nchini Uswiz kufuatia tuhuma za ubadhilifu wa fedha.

Platini pamoja na Blatter waliingia kwenye kundi la watuhumiwa waliofungiwa na FIFA, baada ya serikali ya nchini Usiwz kupata wasi wasi wa malipo ya paund million 1.35 ambayo yanadaiwa kufanywa kwa njia za kifiusadi.

Wengine waliofungiwa na FIFA ni aliyekua katibu mkuu wa shirikisho hilo, Jorome Valke pamoja na aliyekua makamu wa rais Chung Mong-Joon.

UEFA wameafiki jambo hilo kwa kuamini taratibu zilziochukuliwa na FIFA za kumuamuru Platini kukaa pembeni kwa siku 90 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili, upo sahihi kisheria, hivyo halitokua jambo la maana kama wataendelea kufanya kazi kinyume na utaratibu.

Malipo hayo ya utata yanadaiwa kufanywa mwaka 2011, ambapo inadaiwa yalikwenda kwa Platini baada ya kusainiwa na rais wa FIFA Sepp Blatter.

Angalia Orodha Ya Wachezaji Walevi Duniani
CCM Yawataka Wananchi Kutokubali Kubaki Vituoni Kulinda Kura