Msimu wa 2021/22 utaanzisha Mashindano mapya ya vilabu vya UEFA – Europa Conference League pamoja na Europa League kupunguzwa kutoka timu 48 hadi 32 tu, UEFA imeanzisha mashindano ya tatu, ambayo yatafuata muundo sawa na Ligi ya Mabingwa na Europa League.

Europa Conference League ni mashindano ya tatu ya klabu yaliyo chini ya UEFA, sawa kabisa na Ligi ya Mabingwa na Europa League yaliyoanzishwa kwa wazo la kutoa nafasi zaidi kwa vilabu kucheza mashindano ya mpira wa miguu huko Ulaya.

Timu moja kutoka kwa kila ligi tano bora za Ulaya yaani LaLiga, Serie A, Premier League, Bundesliga na Ligue 1 itafuzu kwenye mashindano.

Katika Mataifa yaliyoshika nafasi ya sita hadi 15 katika ubora wa viwango vya Soka yatakuwa na timu mbili zitazoingia, na mataifa yaliyoshika nafasi ya 16 hadi 50 yatakuwa na timu tatu. Timu tatu pia zitaingia kutoka mataifa yaliyoorodheshwa nafasi ya 51 hadi 55, lakini italazimika kupitia raundi zote za kufuzu ili kufanikiwa.

Kutakuwa na raundi tatu za kufuzu na raundi ya mchujo kabla ya timu 32 za mwisho kwenye hatua ya makundi ya Mashindano…. Timu ambazo zitashinda mchujo wao zitafuzu hatua ya makundi, kama vile wale watakaoshindwa kwenye mchujo wa Europa League….Kutakuwa na makundi nane ya timu nne, kama Ligi ya Mabingwa na kama kutoka msimu ujao wa Europa League…

Kila mshindi wa kundi atasonga mbele kwa raundi ya 16. Timu zilizoshika nafasi ya pili zitaingia raundi nyingine ya mchujo dhidi ya timu ambazo zitaangukia kwenye Conference League kutoka kumaliza nafasi ya tatu katika makundi yao ya Europa League. Washindi wa jumla watasonga mbele kukabiliana na washindi wa makundi ya Conference League katika raundi ya 16.

Michezo itachezwa kwa mikondo miwili kabla ya fainali ya mkondo mmoja. Mshindi wa shindano hilo atafuzu kwa msimu ujao wa Europa League; Fainali ya kwanza ya Conference League itachezwa Mei 25, 2022 huko Tirana, Albania.

Kama tu Europa League, mechi za Conference League zitachezwa Alhamisi Jioni.

Watu 6 mbaroni kwa tuhuma kufukua mwili wa marehemu
Kennedy asaini miwili Simba SC