Ukosefu wa uelewa wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 ambayo ipo kwa ajili ya masuala yote ya mtoto, kama vile haki ya mtoto na maslahi yake umetajwa kuwa changamoto katika jamii wakati yanapotokea mafarakano baina ya wazazi, katika kumtunza mtoto.

Akizungumza na Dar24 Media katika kipindi cha mahojiano, Wakili wa kujitegemea kutoka Avis Legal, Henry Mwinuka amesema kumekuwa na changamoto katika utekelezaji wa sheria, huku akitolea mfano kuwa wanaume wengi hudhani akishaachana na mwenza wake anaamini matunzo si lazima.

Amesema kuwa Wanaume wengi wanapenda kutumia mtoto kama fimbo ya kumtesa mama na kuwa swala la mahusiano halihusiani kwa namna yoyote ile na majukumu ya kumlea mtoto kama mzazi, ambapo amesema Sheria ya Kanuni za adhabu, sura ya 16 inasema kuwa kutelekeza au kutokuhudumia mtoto ni kosa la jinai.

Aidha Wakili Henry ameyashauri mashirika mbalimbali na taasisi za kisheria kutokujikita sana katika haki za kisiasa na kusahau kupigia chapuo suala la haki za mtoto kwa kufanya hata kampeni za kuhusu mtoto sio siasa ambayo inakuja kila baada ya miaka mitano.

Hata hivyo ameiomba serikali kuandaa mkakati wa kitaifa wa kupamba na janga hilo kwa kushirikiana na wananchi, wadau mbalimbali, taasisi zisizo za kiserikali na asasi za kisheria, ili kulinda vizazi ambavyo vimebeba maono ya Taifa.

Kumbilamoto: Serikali imefikia muafaka kutatua changamoto hii
Rais Samia kuhudhuria mkutano wa dharura SADC