Kiharusi ni ugonjwa unaotokana na kufa kwa chembe hai za ubongo, ambao husababisha mishipa inayopeleka damu kwenye ubongo kupasuka na kuziba.

Mpasuko wa mishipa hiyo husababisha damu kuingia kwenye ubongo, ambapo hushindwa kuifikia seli za ubongo.

Mbali na mishipa hiyo kupasuka, pia tatizo la kiharusi linaweza kusababishwa na mishipa ya damu kuziba  na kuifanya chembe hai ndani ya ubongo kukosa chakula.

Kutokana na mishipa hiyo kuzibwa na mafuta hupasuka na kusababisha chembe hai ndani ya ubongo kufa kutokana na kukosa chakula ambachoo hupelekwa na damu katika chembe hai na hatimaye kufa na hapo ndipo dalili za kupooza zinapoanza kuonekana.

Matumizi ya mafuta yanaweza kumsababishia mtu Kiharusi baada ya kuingia ndani ya mishipa ya damu na kuvilia, ulaji wa chakula kupita kiasi na kutokufanya mazoezi moja ya sababu ya ugonjwa huu wa kiharusi.

Lakini pia imeelezwa kuwa shinikizo la juu la damu husabisha kiharusi kutokana na mishipa ya damu kupasuka katika ubongo.

Pia watu wenye umri mkubwa wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu kutokana n mishipa yao ya damu kupoteza uimara.

Dalili zinazoonesha uwepo wa ugonjwa wa kiharusi moja wapo ni kuanguka gafla n akupoteza fahamu, kuumwa kichwa, kupata kizunguzungu na kutapika. dalili hizi hutokea kutokana na mshipa unaopeleka damu kwenye ubongo kukatika na kupasuka.

Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani  (WHO), watu milioni 17 hufariki dunia kutona na maradhi ya moyo na kiharusi kila mwaka.

Hivyo watu wananshauriwa kufanya mazoezi mara kwa mara, kupunguza ulaji wa mafuta hasa mafuta yanayotokana na wanyama, lakini pia kuacha ulevi na zinaa.

 

 

 

 

 

 

 

 

Ifahamu vizuri bahati mbaya na visababishi vyake
Serikali kuwaboreshea huduma wastaafu