Gwiji wa klabu ya Newcastle United na timu ya taifa ya England, Alan Shearer amesema anaamini Arsenal watatwaa ubingwa msimu huu.

Staa huyo anayeheshimika nchini England alisema kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na Arsenal hadi sasa, ni wazi wana msimu mzuri.

          Alan Shearer

“Kwa jinsi ninavyoiona Arsenal ya msimu huu nahisi wanaweza kutwaa ubingwa kama wataendelea kukomaa,” alisema Shearer.

Aisema katika msimu uliopita wa 2014/15, Arsenal walikuwa wakifanya vizuri katika mechi moja na kuboronga katika mechi mbili au tatu, jambo lililowarahisishia Chelsea kutwaa ubingwa bila ushindani mkubwa.

Kuhusu kuboronga kwa Chelsea msimu huu, Alan Shearer alisema imetokna na wachezaji kuchoka na baadae kuamua kumkomoa kocha aliyetimuliwa, Jose Mourinho.

Guardiola: Sijajua Ninakwenda Wapi ...
Vinara Wa Ligi Ya La Liga Wafikiria Kumrejesha Shujaa Wao