Waswahili husema utavuna ulichopanda wakiwa na maana baada ya kazi uliyofanya basi utakachopata ndicho ambacho unastahili na hii ni baada ya Baraza la Mitihani Tanzania  kutangaza matokeo ya ufaulu wa kidato cha sita kushuka kwa asilimia 0.93% kutoka asilimia 98.87 mwaka jana kufika 97.94.

Akitoa taarifa leo kwa wanahabari Katibu mtendaji (Necta) Dkt Charles Msonde amesema ufaulu umeshuka huku ubora wa ufaulu ukiwa unazidi kuimarika kwa kuwa idadi kubwa ya waliofaulu katika daraja la I, II na III umeongezeka kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka iliyopita.

Dkt Msonde amesepia pia ufaulu wa masomo ya sayansi umeshuka  ukilinganisha na mwaka jana kutoka 8.9 hadi 5.3 huku upande wa masomo ya biashara ukishukuka kutoka 6.9 mpaka 1.7 mwaka huu.

Hata hivyo amesema katika matokeo ya ufaulu kitaifa mikoa ya Arusha, Dar es Salaam pamoja na Pwani ndizo zilizotamba katika shule  kumi bora huku shule za serikali zikiwa hazipo nyuma sana.

Vile vile baraza limezuia matokeo ya wanafunzi 25 waliokutwa na makosa ya udanganyifu katika mitihani ikiwa ni pamoja na kukutwa wakitumia simu kwenye mitihani kupata majibu na wengine wakiwa na majibu (nondo).

Aidha Dkt Msonde amefafanua kuwa jumla ya wanafunzi 10 ambao hawakumaliza kufanya baadhi ya mitihani kutokana na matatizo ya kiafya na 36 ambao hawakufanya kabisa kutokana na sababu hizo watapewa fursa ya kufanya mitihani mei 2017.

Mtihani wa kidato cha sita ulifanyika Mei 02 -19 ambapo jumla ya wanafunzi 74,896 wa shule  na wanaojitegemea  walifanya mitihani hiyo huku wanafunzi 309 wakishindwa kufanya kabisa mitihani hiyo..

 

 

Fid Q kuandaa Script ya Wimbo Mpya wa Bella
Video: Polisi Dar wakamata Genge la 'Panya road', Bunduki ya kienyeji