Ufisadi unaodaiwa kufanywa na mshindi wa taji la Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare umepelekea serikali ya awamu ya tano kuiadhibu benki ya Stanbic kwa kuitoza faini ya shilingi bilioni 3.

Mrembo huyo wa Tanzania alihusishwa na ufisadi kwa kufanya miamala kupitia Benki ya Stanbic kinyume cha sheria na kuwezesha malipo kwa Kampuni ya Kitanzania ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA) kati ya mwaka 2012 alipokuwa Afisa Mwandamizi wa benki hiyo.

Ukaguzi uliofanywa ulibaini kuwa Shose alishirikiana na aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bashiri Awale kufanikisha muamala huo wa kifisadi uliofanyika baada ya Benki ya Stanbic kushiriki katika kuwezesha mkopo wa serikali wa Dola za kimarekani Milioni 600.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango alieleza kuwa dola milioni 6 ziliwekwa katika akaunti ya EGMA kupitia benki hiyo na kutolewa ndani ya muda mfupi kwa fedha taslim kinyume cha sheria.

“Jumla ya malipo yalikuwa dola milioni 6 za Marekani na zililipwa katika akaunti ya EGMA na kutolewa kwa muda mfupi kwa njia ya fedha taslimu. Hii ni nje ya taratibu za kibenki,” alisema Dk. Mpango.

Dk. Mpango alieleza kuwa baada ya Benki Kuu kufanya ukaguzi na kujiridhisha kuwa benki hiyo ilikiuka taratibu za kibenki kwa makusudi imeiandikia barua benki hiyo kujieleza kwa nini isitozwe faini hiyo. Alisema endapo Benki Kuu ya Tanzania haitaridhishwa na utetezi wa benki hiyo italazimika kulipa faini tajwa.

Hadji Mwinyi: Udhaifu Wa Oscar Joshua Ndio Mtaji Wangu
Van Gaal Aanza Mbwembwe Baada Ya Kuifunga Liverpool