Haruna Juma – Katavi.

Wafugaji Mkoani Katavi wametakiwa kuachana na ufugaji wa kizamani wa kuhamahama na mifugo, badala yake wafuge kwa kuzingatia mbinu za kisasa za ufugaji zenye tija.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko kwenye kikao cha wadau wa sekta ya mifugo kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa mjini Mpanda.

Amesema, kumekuwa na migogoro baina ya wafugaji na wakulima ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na wafugaji kuhamahama na mifugo yao hivyo kama zitatumika mbinu za kisasa kutakomesha migogoro hiyo.

Aidha ameziagiza halmashauri zote za mkoa wa Katavi kuhakikisha zinatengeneza mazingira wezeshi kwa wafugaji ikiwemo kutoa elimu kuhusu mbegu bora, madawa na chanjo za mifugo yao. 

Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa wafugaji waliohudhuria kikao hicho wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu zaidi kuhusu nyanda maaluma za malisho zilizotengwa na serikali kwani kuna baadhi ya watu wasio na nia njema wameanza kuvamia na kuanzisha shughuli zingine tofauti na lengo la ufugaji. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Mifugo wakiwemo Wakuu wa waziri Wilaya za Mpanda na Tanganyika, wazalishaji wa madawa na chanjo za mifugo, wasindikaji wa mazao ya mifugo na viongozi wa chama cha wafugaji.

Msimamo ni kuhamasisha ujenzi wa Viwanda - Majaliwa
Habari ya kushangaza Dodoma