Bao la Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Ally Samatta dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati limemkosha Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Polusen.

Taifa Stars jana Jumatano (Machi 23) ilicheza Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ma kupata ushindi wa 3-1.

Kocha Kim alikiri kufurahishwa na bao hilo, alipozungumza na Azam TV baada ya mchezo huo ambapo alisema kwa muda mrefu hajaona aina ile ya bao likifungwa kwa ustadi mkubwa na jinsi lilivyotengenezwa kwa kupigwa pasi kutokea nyuma.

“Wakati wangu bora kwenye mchezo wa leo ni bao la pili, kwa muda mrefu sijaoana aina hii ya mpira na pasi, kwa kweli ulikuwa wakati mzuri.” Alisema Kim

Bao hilo lilifungwa dakika ya 62 ya mchezo ambapo mashambulizi yalianzia kwa mlinzi wa kati Bakari Nondo Mwamnyeto na kupigwa jumla ya pasi nne mpaka kumfikia mfungaji.

Aidha kocha huyo aliendelea kusema kuwa amejivunia nafasi kikosi chake kwa kutengeneza nafasi nyingi kwa aina ya timu ngumu kama Afrika ya kati jambao ambao limetia faraja.

“Tumetengeneza idadi kubwa ya nafasi, tumefunga mabao matatu, ukiangalia kwenye kwenye ushambuliaji ninafuraha kutengeza idadi nyingi za nafasi dhidi ya mpinzani kama Afrika ya kati, ambao ni timu nzuri na ngumu na wanacheza vizuri.” Alisema kocha huyo

Mabao mengine ya Taifa Stars kwenye mchezo huo yalifungwa na Novatus Dismas pamoja na Mshambuliaji wa Geita Gold FC George Mpole.

Pascal Wawa awatuliza mashabiki Simba SC
Zakazakazi: Hatuiogopi Young Africans, Mayele wa kawaida sana