Mgombea Urais na Kiongozi wa Chama cha National Unity Platform (NUP),Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu kwa jina la Bobi Wine, amekamatwa na jeshi la Polisi nchini humo leo Novemba 18 ,2020 akiwa katika harakati zake za kufanya kampeni.

Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki, amekamatwa kufuatia mzozo kati ya wafuasi wake na watendaji wa usalama katika eneo lake la kampeni.

Inaelezwa kuwa ukamatwa kwa Mwanasiasa na mwanamuziki huyo kunakuja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Martin Okoth Ochola kumuonya kwamba amekuwa akikaidi miongozo ya uchaguzi yenye nia ya kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa wa COVID-19.

“Licha ya maonyo yanayotolewa mara kwa mara kwa wagombea, mawakala wao na umma kwa ujumla juu ya athari mbaya na hatari za kiafya za kufanya mikutano na maandamano yasiyoruhusiwa, tunaendelea kushuhudia vitendo vya kukaidi na kupuuza kabisa miongozo ya EC, kwahivyo wale watakaokaidi miongozo hii ya Tume ya Uchaguzi na mipango yao mibaya inayolenga kuvuruga mchakato wa uchaguzi watawajibishwa”, amesema IGP Ochola.

Bobi Wine ambaye yupo katika harakati zake za za kutaka kumuondoa Rais wa Yoweri Museveni ambaye ameliongoza Taifa hilo tangu mwaka 1986.

DRC yatangaza kumalizika kwa Ebola
TFF yabariki usajili wa kimataifa Simba SC