Mchezesha Muziki Nchini Uganda amepatwa na mauti baada ya kuvamiwa na kundi la vijana waliompiga kwa kosa la kuweka wimbo ambao hawakuupenda walipokuwa wanacheza muziki kwenye ukumbi mmoja uliopo wilayani Nebbi nchini humo.
Dj Jerry Okirwoth alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Parombo, alikuwa anajitolea kufanya kazi ya U-DJ muda wa usiku baada ya masomo yake ili kujipatia kipato cha kumudu mahitaji yake ya shule.
Kamishna wa Polisi wa wilaya ya Nebbi, William Bob Labeja amethibitisha kutokea kwa kifo hicho, ambapo amesema kuwa mwanafunzi huyo aliuawa siku ya Jumatano na ameulaumu uongozi wa ukumbi uliotumika na wauaji hao kwa kushindwa kumlinda marehemu kabla hajapatwa na mauti.
“Nikiwa kama kiongozi Mkuu wa usalama katika wilaya hii sitaruhusu kumbi za muziki kuendelezwa na nazitaka kumbi zote zifungwe kwani zimekuwa hatari kwa maisha ya vijana,” amesema Bob Labeja
Kwa upande wake mwenyekiti wa eneo hilo, Bosco Okwai amesema kuwa mwaka 2011 walitengeneza sheria inayozuia vibali vya kuendesha kumbi za Muziki na amewataka viongozi wote wa mitaa kuhakikisha wanawapeleka mbele ya sheria watu wote watakao ipuuza sheria hiyo.
-
Video: Mapya ya ugaidi Kenya, Kuna giza nene uchaguzi ujao
-
Nairobi: Aliyenusurika shambulizi la Osama ni miongoni mwa waliouawa
-
Abiria 36 watekwa nyara Cameroon