Raia wa Uganda zaidi ya Milioni 18 wanatarajiwa kushiriki kupiga kura katika Uchaguzi mkuu unaofanyika hii leo Januari 14, 2021 nchini humo kumchagua rais na wawakilishi wapya wa bunge .
Katika uchaguzi huo Rais Yoweri Museveni, ambaye anatetea wadhifa wake anakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa mwanamuziki Robert Kyagulanyi Ssentamu maarufu kama Bobi Wine.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo Jaji Simon Byabakama, amesema kwamba wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni tisa na jinsia ya kike wakiwa zaidi ya milioni tisa.
Bobi Wine ni mgombea ambaye amevutia idadi kubwa ya vijana nchini humo.
Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Hata hivyo rais Museveni anajivunia utawala wake wa muda mrefu ambapo amefanya baadhi ya maenedeleo katika nchi hiyo.
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.