Katika kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za majini ambazo zimekuwa zikitokea mfululizo katika nchi za Afrika Mashariki, Serikali ya Uganda imeamua kukabiliana na janga hilo kwa kutenga bajeti itakayo husisha ununuzi wa boti za wagonjwa (Boat ambulances).
Waziri wa Afya Nchini Uganda, Dkt. John Nambohe amesema kuwa katika bajeti yake ya mwaka 2019/2020 ameupa kipaumbele mpango wa ununuzi wa boti za wagonjwa ili kuimarisha huduma za dharula za nchi hiyo hasa upande wa uchukuzi wa majini.
Akitoa ufafanuzi wa bajeti hiyo, Nambohe ameeleza kuwa kumekuwa na uzembe mkubwa katika huduma ya dharula ya majini hivyo kupelekea vifo vya watu wengi pale ajali zinapotokea na kukumbushia ajali ya hivi karibuni iliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 30.
“Tutaanza kwa kusambaza boti chache katika vijiji 20 ambavyo vimezungukwa na maji katika nchi yetu ili kurahisisha huduma za dharula” amesema Dkt. Nambohe
Hata hivyo, miongoni mwa vijiji vilivyo zungukwa na maji ambavyo vitapewa boti za wagonjwa nchini Uganda ni pamoja na Buvuma, Jinja, Buikwe, Masaka, Hoima, Buliisa, Ntoroko, Mukono, na Namayingo.
-
Mtolea aanza kuuvizia ubunge, asema hana ugomvi na wabunge wa upinzani
-
Vigogo watano wa WETCU watupwa jela
-
LIVE: Rais Magufuli na Waziri Mkuu Misri wakishuhudia utiaji saini ujenzi wa mradi wa umeme Rufiji