Uganda imeamua kuwaondoa wanajeshi wake kutoka nchini Somalia ifikapo mwezi Disemba mwaka 2017.

Uganda inachangia wanajeshi wengi zaidi kwa kikosi cha muungano wa afrika kinachopigana na wanamgambo wa Al-Shabab.

Mkuu wa jeshi nchini Uganda Jenerali Katumba Wamala, aliiambia BBC kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na hujuma kutoka kwa jeshi la Somalia na washirika wa kimataifa.

Marekani, Uingereza na Uturuki ni kati ya nchi ambazo hutoa mafunzo kwa jeshi la polisi wa Somalia.

Lakini serikali ya Uganda inasema kuwa nchi hizo hazitoi ushirikiano.

Jenerali Wamala anasema kwa Uganda itaondoa jeshi lake kabla ya Disemba mwaka 2017 ikiwa nchi nyinge itapatikana kuchukua mahala pake.

Video: 'Nipo pamoja na wanasiasa na atashirikiana nao vyema' - Rais Magufuli
Wanajeshi Wa Sudan Kusini Waiba Chakula