Uganda inaomboleza kifo cha Sokwe anayejulikana kwa jina la Zakayo ambaye ni mkubwa kuliko wote nchini humo aliyefariki akiwa na umri wa miaka 54.
Zakayo ambaye alizaliwa mwaka 1963 alikuchukuliwa na Kituo Cha Elimu ya Hifadhi Wanyamapori nchini humo akiwa na umri wa miaka 13 na kupelekwa katika hifadhi ya Entebe.
Aidha, Zakayo ambaye alikuwa akiitwa ‘Babu’ wa Sokwe wote nchini Uganda aliishi kwa furaha katika hifadhi hiyo.
Wataalam wa hifadhi wamemsifu Zakayo kwa kuwa balozi wa Sokwe na wanyama wengine nchini Uganda, ambapo wasifu wake ulisaidia kujipatia fedha kwa juhudi za uhifadhi na kuongeza idadi ya watalii.
Hata hivyo, wanyama hao wengi wako kwenye maeneo yasiyo na usalama, ambapo huwa hatarini kuuawa na majangili, Ebola na uharibifu wa mazingira.