Serikali nchini Uganda imetangaza kuwa itawaachilia huru wafungwa 170 wa Rwanda ambao wanashikiliwa katika Magereza ya nchi hiyo.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Rwanda, Vincet Biruta jana amethibitisha taarifa hiyo na kusema kuwa ni hatua nzuri katika kuboresha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.
“Uamuzi huo wa Uganda ni hatua moja mbele katika kutekeleza makubaliano ya Luanda Angola yaliyotiwa saini baina ya marais wa nchi hizo mwaka jana” amesema waziri Biruta.
Ikumukwe kuwa, Februali mwaka jana, Rwanda ilifunga mpaka wake na Uganda kwa kuituhumu kuwa imekuwa ikiwatesa na kuwafunga watu wake kinyume na sheria.
Jambo ambalo Uganda nayo iliituhumu Rwanda kwa kufanya ujasusi katika aridhi yake.
Agosti mwaka jana, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais Paul Kagame walisaini makubaliano ya amani katika mji mkuu wa Angola, Luanda yaliyolenga kumaliza uhasama uliopo baina ya mataifa hayo mawili.